HIVI NDIVYO ANKO MAGU ALIVYO GONGA MSUMARI VITA YA MAKONDA DHIDI YA WATUMIAJI NA WAUZAJI WA DAWA ZA KULEVYA








Rais Magufuliakizungumza baada ya kuwaapisha Mkuu wa Majeshi, Kamishna wa Magereza, Mnadhimu Mkuu na Mabalozi.

DAR ES SALAAM: Siku chache baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makondakujitosa kwenye vita ya madawa ya kulevya kwa kuagiza wasanii, wafanyabiashara na askari wanaodaiwa kuhusika na utumiaji na biashara ya madawa ya kulevya wajisalimishe kituo kikuu cha polisi kwa mahojiano, huku wengine wakiwa tayari wameshaanza kuchukuliwa hatua, Rais Magufuli amempongeza kwa hatua hiyo na kumtaka aendelee kuwakamata wahusika wote.


Rais Magufuliakizungumza baada ya kuwaapisha Mkuu wa Majeshi, Kamishna wa Magereza, Mnadhimu Mkuu na Mabalozi.

Raia Magufuli, amesema anafurahishwa na namna Makonda anavyofanya kazi hiyo na kutaka aendelee kuwakamata, bila kujali umaarufu au cheo cha mtu na kuwataka viongozi wengine kuungana naye kuhakikisha wahusika wote wa biashara ya madawa ya kulevya, wanakamatwa na kufikishwa mbele ya sheria. Akaongeza kuwa watumiaji wakikamatwa, wabanwe ili wawataje wanaowauzia mpaka kuwafikia wauzaji wakubwa.



Rais Magufuli ameyazungumza hayo katika hafla ya kuapishwa kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo, Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa na Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Luteni Jenerali James Mwakibolwa pamoja na mabalozi wa Tanzania nchini Ufaransa na DRC.


Rais Magufuli akisalimiana na IGP Mangu.

Pia Rais Magufuli amemuagiza kaimu jaji mkuu wa Tanzania, kuhakikisha kesi za madawa ya kulevya, zinasikilizwa haraka na kutolewa hukumu ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaoshiriki kwenye biashara hiyo inayomaliza nguvu kazi ya taifa.

Rais Magufuli alikumbushia kesi ya mfanyabiashara wa madawa ya kulevya aliyekamatwa Mtwara, Shikuba ambaye licha ya kukamatwa siku nyingi zilizopita, bado hajapandishwa mahakamani na kuitaka idara ya mahakama, kushughulikia suala hilo haraka.

Mabli na hivyo, Rais Magufuli amempongeza IGP Mangu kwa kuwasimamisha kazi Askari 12 wanaotuhumiwa kujihushisha na biashara ya dawa za kulevya na kusema kuwa vita hiyo siyo ya RC Makonda pekee bali ni ya Watanzania wote.



ALICHOKISMEA RAIS MAGUFULI

Vita ya dawa za kulevya haina cha umaarufu, haijalishi ni mtoto wa nani anahusika, hata kama ni mke wangu mkamateni

Najua IGP kuna watu walikupigia simu wanakupa ushauri kuhusu dawa za kulevya, ungewasikiliza leo usingekuwa ni IGP- Rais Dkt @MagufuliJP

Ombi langu ni Tanzania ya viwanda ionekane kwenye majeshi yetu, haiwezekani hadi leo tunaagiza sare kutoka nje ya nchi- Rais Dkt @MagufuliJP

Kuna mfanyabiashara maarufu wa dawa za kulevya alikamatwa mkoani Lindi lakini sijawahi kusikia amefikishwa mahakamani, its too much- Rais @MagufuliJP

Hawa wakubwa wakubwa tuwashughulikie badala ya kusumbuka na hawa wadogo wadogo. -Rais@MagufuliJP
SHARE

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment